Chris na Moeen kuikosa Afghanistan

Image caption Mchezo wa Kriket

Wachezaji Chris Woakes na Moeen Ali wameenguliwa katika kikosi cha timu ya kriket ya England sababu ya majeruhi.

Wachezaji hao watakosa mchezo wa kukamilisha ratiba dhidi ya Afghanistan ambapo timu zote zimeshatolewa kwenye michuano ya kombe la dunia.

Woakes anasumbuliwa na maumivu ya mfupa wa mguu huku Moeen akiwa na tatizo la misuli kwenye upande wa kushoto wa tumbo.

England walitupwa nje ya michuano dunia ya kriket baada ya kupoteza mchezo wa jumatatu dhidi ya Bangladesh.