James Ward atinga hatua ya pili

Image caption Davis Cup mashabiki wakifuatilia

Mcheza tenesi namba mbili kwa ubora nchini England James Ward ametinga hatua ya pili ya michuano ya wazi ya (BNP Paribas).

Ward amemfunga Mitchell Krueger wa marekani kwa seti 2-6 6-3 7-6 (7-0).

Ushindi huu umekua ni ushindi muhimu kwa Ward, baada ya kumshinda mchezaji John Isner anayeshika nafasi ya 20 kwa ubora wa dunia wiki iliyopita kwenye michuano ya Davis Cup.

Mchezaji huyo ameingia kwenye kundi la wachezaji bora 100 wa mchezo wa tenesi kwa mara ya kwanza na atapambana na mchezaji nyota wa ujerumani Mischa Zverev, kwenye hatua inayofuata.