Ujumbe wa kibaguzi kwa Welbeck wachunguzwa.

Haki miliki ya picha
Image caption Danny Welbeck akifurahia jambo

Polisi katika mji wa Manchester wanafanya uchunguzi kusuhu ujumbe wa kibaguzi katika mtandao wa kijamii wa twitter kumuendea mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck.

Ujumbe ulikuja kufuatia Welbeck kufunga bao la ushindi la Arsenal dhidi ya klabu yake ya zamani ya Manchester United katika robo fainali ya Kombe la FA Jumatatu iliyopita.

Vita dhidi ya ubaguzi ulaya haswa kwenye michezo bado inaonekana kuwa ngumu baada ya tabia hizo kuendelea kukithiri

hivi karibuni mashabiki wa Chelsea walinaswa katika picha za video wakimzuia mtu mweusi kuingia katika treni jijini Paris.