Mbio za Dunia za Nyika March 28,2015

Image caption Mbio za dunia za nyika ni March 28,2015

Wachezaji wa riadha wa Tanzania wameweka kambi ya mazoezi mkoani Arusha, Kaskazini mwa Tanzania na kufanya mazoezi makali kwa ajili ya matayarisho ya kushiriki mbio za Nyika za dunia zitakazofanyika China Machi 28.

Chama cha riadha nchini Tanzania kimesema wanariadha wake wanaendelea vizuri na mazoezi chini ya kocha Francis John.

Kikosi cha wanariadha waliochaguliwa kinahusisha wale ambao walifanya vizuri dhidi ya Kenya katika mbio fupi (half marathon) za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi, Kilimanjaro.

Kenya ilitawala katika mbio ndefu (full Marathon) kwa kushinda kumi bora zote katika mbio hizo za Kilimanjaro Marathon.

Wakimbiaji wanaofanya mazoezi Arusha ni Fabian Nelson na Bazi John kutoka chuo cha Polisi cha Moshi.

Wengine ni Alphonce Erick wa Arusha, Emmanuel Giniki na Joseph Theophil.