Nigeria imefuzu kwa kombe la dunia la U20

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nigeria imefuzu kwa kombe la dunia la wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20.

Nigeria imefuzu kwa kombe la dunia la wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20.

Flying Eagles ya Nigeria ilijikatia tikiti hiyo ya moja kwa moja baada ya kufuzu kwa nusu fainali ya mashindano ya kuwania kufuzu .

Vijana hao chipukizi wa Nigeria waliwalaza Congo mabao 4-1 katika mechi yao ya pili ya kundi A iliyochezwa Senegal.

Washiriki wote wa hatua ya nusu fainali ya mashindano haya ya Afrika wanafuzu kuiwakilisha bra la Afrika kwatika Fainali za dunia zitakazochezwa mwezi Mei na juni mwaka huu kule New Zealand.

Nahodha wao Musa Muhamed alifunga mabao mawili huku Ifeanyi Matthewna mchezaji aliyetuzwa kwa kuwa mchezji bora katika mechi hiyo Taiwo Awoniyi akikamilisha kichapo hicho kilichowahakikishia nafasi ya kushiriki fainali za kombe la Dunia.