Serena akumbuka alivyodhalilishwa 2001

Haki miliki ya picha none
Image caption Serena Williams

Mcheza tenis mwanadada namba moja kwa ubora duniani Serena Williams amesema haamini kama anaweza kurejea mji Indian Wells huko Calfonia nchini Marekani kushiriki mashindano ya tenis baada ya kudhalilishwa na watazamaji wakati alipokuwa msichana wa miaka 19.

Serena ambaye kwa sasa ana miaka 33 huenda akashiriki tena mashindano ya BNP Paribas Open yatakayofanyika katika mji Califonia baada ya kuyasusia kwa miaka 14.