Man United kumkosa Di Maria

Haki miliki ya picha PA
Image caption Manchester United kumkosa nyota wake Angel Di Maria

Klabu ya Manchester United itamkosa Angel Di Maria,ambaye anatumikia adhabu ya kukosa mechi moja baada ya kupewa kadi nyekundu dhidi ya Arsenal.Naye Jonny Evans anatumikia adhabu kama hiyo.

Mshambuliaji nyota Robbin Van Persie bado anauguza jeraha huku Marcos Rojo akiwa hajulikani iwapo atachezeshwa kutokana na jeraha la paja.

Hata hivyo Ashley Young atacheza licha ya kuumia mguu siku ya Jumatatu.

Kocha wa klabu ya Tottenham Mauricio Pochettino ana kikosi chake kizima.

Danny Rose huenda akacheza mechi ya leo katika safu ya ulinzi wa kushoto huku Mousa Dembele pia akitarajiwa kuanza.