Dick Advocaat ateuliwa kocha Sunderland

Image caption Advocaat amekuwa bila kazi tangu ajiuzulu kama kocha wa Serbia mwezi Novemba.

Siku moja baada ya kumtimua wake Gus Poyet klabu inayoshiriki ligi kuu ya Premia ya Uingereza ,Sunderland imemuajiri Dick Advocaat kama mkufunzi mkuu wa timu hiyo hadi mwisho wa msimu.

Mkufunzi huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi anachukua hatamu wakati ambao ''the Black Cats'' wanachungulia upanga wa kuwashusha daraja .

Mwenyekiti wa klabu hiyo bwana Ellis Short amesema kuwa kocha huyo mpya anafahamu fika wajibu wake

''kuisaidia Sunderland kusajili alama na kuzuia isishushwe daraja msimu ujao''.

Advocaat, mwenye umri wa miaka 67,aliwaambia waandishi wa habari kuwa yuko tayari kuanza kazi yake.

Gus Poyet:

Advocaat anachukua pahala pa Poyet, 47, aliyefahamishwa hatima yake jumatatu tarehe 16 machi baada ya zoezi la siku na mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo Margaret Byrne.

Raiya huyo wa Uruguay alishika hatamu Sunderland baada ya Paolo Di Canio kuondoka ''Stadium of Light'' mwezi Oktoba 2013.

Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Brighton aliiongoza Sunderland kusajili ushindi katika mechi nne akatoka sare katika mechi sita za mwisho na hivyo kuihakikishia timu hiyo nafasi yake katika ligi guu msimu huu.

Atakumbukwa kwa kuiongoza Sunderland kuibana Chelsea na Manchester United kabla ya kutoka sare na Manchester City.

Poyet vilevile aliiongoza Sunderland kuingia katika fainali ya 2014 ya Capital One Cup.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Sunderland imemuajiri Dick Advocaat kama mkufunzi mkuu wa timu hiyo hadi mwisho wa msimu.

Hata hivyo kocha huyo mgeni amesema kuwa ''Sunderland ni klabu kubwa ambayo anafahamu haitakuwa rahisi kuinusuru''

"la muhimu kwa sasa ni kumakinikia mechi ya jumamosi hii''

Advocaat amekuwa bila kazi tangu ajiuzulu kama kocha wa Serbia mwezi Novemba.

Kocha huyu kutoka Uholanzi anajivunia tajriba kubwa akiwa amewahi kuhudumu katika wadhifa huo akiwa Rangers, PSV Eindhoven na Zenit St Petersburg.

Aidha Advoocat aliwahi kuifunza timu ya taifa ya, Ubejiji Korea Kusini, mbali na kutwaa mataji makuu ya ligi ya uholanzi , Scotland na Urusi.

Atasaidiwa katika wadhfa huo na Zeljko Petrovic huku aliyekuwa kocha wa walinda lango wa swanswea Adrian Tucker akichukua hatamu kama mkufunzi wa makipa.