Sunderland yamtimua Gus Poyet

Haki miliki ya picha PA
Image caption Raiya huyo wa Uruguay alishika hatamu Sunderland ''Stadium of Light'' mwezi Oktoba 2013.

Klabu ya ligi kuu ya Uingereza Sunderland imemtimua kocha Gus Poyet kufuatia msururu wa matokeo duni.

Sunderland imesajili ushindi mmoja pekee kati ya mechi 12 za ligi kuu ya Premia.

The Black Cats wamesalia nje tu ya eneo la hatari ya kushushwa daraja hasa baada ya kuambulia kichapo cha mabao 4-0 siku ya jumamosi mikononi mwa Aston Villa.

"inatupa huzuni kubwa kuwa tumeshindwa kusajili matokeo tuliyotazamia kabla ya mwisho wa mpaka wetu alisema Mwenyekiti wa klabu hiyo Ellis Short.

"Kwa hakika hatukutarajia kuwa tutakuwa tukipigania upande wa mwisho wa ligi kama tunavyofanya kwa sasa .Bila shaka tunahitaji mabadiliko ilikuinusuru klabu yetu''

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Klabu ya ligi kuu ya Uingereza Sunderland imemtimua Gus Poyet kufuatia msururu wa matokeo duni

Klabu hiyo ya Sunderland imetoa taarifa ikisema kuwa meneja atakayemrithi Poyet atatangazwa karibuni.

Hali sasa ni tete kwao wakijiandaa kuchuana dhidi ya West Ham bila ya mkufunzi siku ya jumamosi.

Aidha Sunderland itakabiliana Newcastle tarehe 5 Aprili.

Rekodi ya Gus Poyet akiwa Sunderland

Poyet, 47, alifahamishwa hatima yake baada ya zoezi la siku ya jumatatu na mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo Margaret Byrne.

Haki miliki ya picha d
Image caption Atakumbukwa kwa kuiongoza Sunderland kuibana Chelsea na Manchester United

Raiya huyo wa Uruguay alishika hatamu Sunderland baada ya Paolo Di Canio kuondoka ''Stadium of Light'' mwezi Oktoba 2013.

Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Brighton aliiongoza Sunderland kusajili ushindi katika mechi nne akatoka sare katika mechi sita za mwisho na hivyo kuihakikishia timu hiyo nafasi yake katika ligi guu msimu huu.

Atakumbukwa kwa kuiongoza Sunderland kuibana Chelsea na Manchester United kabla ya kutoka sare na Manchester City.

Poyet vilevile aliiongoza Sunderland kuingia katika fainali ya 2014 ya Capital One Cup.