Facebook:Ronaldo ndiye binadamu maarufu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mchezaji nyota wa Real Madrid ya uhispania na Ureno christiano Ronaldo ndiye binadamu maarufu zaidi kwenye Facebook.

Mchezaji nyota wa Real Madrid ya Uhispania na Ureno Christiano Ronaldo ndiye binadamu maarufu zaidi duniani kwenye Facebook.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 amempiku Mwanamuziki maarufu kwa kunengua kiuno Shakira nawafuasi zaidi ya milioni 107.

Ronaldo anawafuasi 107,096,356 wakilinganishwa na 107,087,100 Shakira

Ronaldo aliweka rekodi kwa kuwa mchezaji maarufu zaidi duniani alipotimiza wafuasi milioni 100 mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Nyota huyo wa Real Madrid alijiunga na mtandao wa kijamii wa Facebook mwaka wa 2009.

Na si hapo alikodhibitisha udedea wake, Ronaldo anazaidi ya wafuasi milioni 34 katika mtandao wa kijamii wa Twitter ambako anaorodheshwa katika nafasi ya 13.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ronaldo anawafuasi 107,096,356

Msanii h Katy Perry ndiye anayeongoza kwa umaarufu kwenye twitter akiwa na jumla ya wafuasi milioni 66.6.

Justin Bieber, Barack Obama, Taylor Swift, YouTube, Lady Gaga, Justin Timberlake, Rihanna, Britney Spears, Ellen DeGeneres, Instagram na Twitter ndio wanaompiku Ronaldo.

Licha ya hiyo yeye ndiye mwanaspoti maarufu zaidi kwenye mtandao huo wa Twitter.

Mshambulizi wa Brazil na Orlando City Kaka ndiye mchezaji wa pili kwa umaarufu akiwa na wafuasi milioni 22.2 million.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ronaldo ndiye mchezaji maarufu zaidi duniani

Licha ya kuwa maarufu na wafuasi wa timu ya Uingereza ya Manchester United kiungo machachari Wayne Rooney anashikilia nafasi ya 95 katika mtandao huo akiwa na wafuasi milioni 10.8 million.

Katika Facebook hata hivyo, Mchezaji bora mara nne duniani na Mshambulizi wa Barcelona ,Lionel Messi ndiye mwanaspoti wa pili kwa umaarufu duniani.

Messi anawafuasi milioni 78.

Nyota wa zamani wa England David Beckham anafunga orodha ya tatu bora kwa wafuasi milioni 52 .