Tanzania yawafunga wageni katika kriketi

Nahodha wa timu ya taifa ya kriketi ya Tanzania, Hamis Abdallah alifunga runs 45 na kuiwezesha timu yake kuifunga timu ya wachezaji wa kigeni kwa runs 14 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika klabu ya Dar es Salaam Gymkhana.

Mechi hiyo ina lengo la kuiandaa timu ya Tanzania kwa ajili ya michuano ya Afrika Daraja la 1 nchini Afrika ya kusini baadae mwezi huu.

Pia ina lengo la kujiandaa na michuano ya ligi ya APL, ambapo wachezaji wa kigeni 12 kutoka nchi za India, Pakistani, Afrika ya Kusini na Uingereza wamealikwa kwa kushiriki ligi hiyo ili kuwapa uzoefu wachezaji wazawa.

Wenyeji walishinda tosi na kushinda 150 all out (wote nje) katika ova ya 38.1 .

Max Osbone kutoka Afrika ya Kusini alipata runs 48 kwa upande wa wachezaji wa kigeni.

Michuano ya APL imeanza Alhamisi katika viwanja tofauti na kila timu shiriki itakuwa na wachezaji wa kigeni watatu ili kuleta ushindani.