Timu ya soka la ufukweni kuelekea Misri

Image caption Soka la ufukweni likipigwa

Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Beach Soccer) inatarajiwa kuondoka siku ya alhamisi, kuelekea jijini Cairo nchini Misri,

kwa ajili ya mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa soka la ufukweni utakaofanyika siku ya jumapili.

Tanzania inapaswa kupata ushindi katika mchezo wa marudiano dhidi ya Misri utakaofanyika siku ya jumapili jijini Cairo ili kufuzu kwa fainali za soka la ufukweni barani Afrika zitakazofanyika visiwa vya Shelisheli kufuatia kupoteza mchezo wake awali.

Msafara wa timu ya Beach Soccer utakaoondoka na shirika la ndege la Ethiopia, utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Ahmed Msafiri Mgoyi, kocha mkuu John Mwansasu, kocha msaidizi Ali Sheikh Alhashby, meneja Deogratius Baltazar na daktari wa timu Dr Leonidas Rugambwa.