Sepp Blatter akataa mjadala na wapinzani

Haki miliki ya picha
Image caption Sepp Blatter

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amekataa ombi la pamoja kutoka mashirika ya habari ya BBC na SKY kushiriki katika mjadala utakaokwenda hewani moja kwa moja.

Wapinzani wake watatu wamekubali kushiriki katika mjadala huo lakini wakasisitiza kuwa wagombea wote ni sharti washiriki katika mjadala huo kama mojawapo ya masharti.

Mapendekezo hayo ya BBC na SKY yaliwalenga mashabiki ambao wamesema kuwa wanataka kuwauliza maswali wagombea hao.

Uchaguzi wa rais wa shirikisho la FIFA unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 29 mwezi Mei mjini Zurich.

Wagombea wengine katika uchaguzi huo wa FIFA ni rais wa shirikisho la soka nchini Jordan Ali Bin Al Hussein,Rais wa shirikishp la soka nchini Uholanzi Michaek Van Praag na aliyekuwa mchezaji wa Barcelona Louis Figo.

Blatter mwenye umri wa miaka 79 anataka kuliongoza shirikisho hilo kwa muhula wa tano.