NIC yatesa :netball Afrika Mashariki

Image caption Kazi ya kutetea ubingwa

Mabingwa watetezi wa michuano ya mpira wa pete kwa nchi za Afrika ya Mashariki, NIC ya Uganda inatetea vema ubingwa wake baada ya kuendeleza ushindi katika michuano inayoendelea Zanzibar.

NIC iliifunga timu ya Prisons ya Uganda kwa magoli 35-32 katika viwanja vya Gymkhana.

NIC inaongoza kundi A ikiwa na pointi 8, huku ikiweka rekodi ya kutopoteza mechi.

MOICT ya Kenya inaongoza kundi B ikifuatiwa na KCCA ya Kenya, ambayo iliifunga Uhamiaji kwa mabao 52-38.

Michuano hiyo inashirikisha timu za Zanzibar, Kenya, Uganda na Tanzania Bara.

Mashindani yaliyopita yalifanyika Dar es Salaam na timu ya Bima ( National Insurance Corporation-NIC) ya Uganda iliwafunga JKT Mbweni ya Tanzania Bara katika fainali na kuchukua ubingwa kwa upande wa wanawake.