Muda wa pellegrin umekwisha- Savage.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Manuel Pellegrini

Mchambuzi wa mchezo wa soka wa BBC, Ribbie Savage amemtabiria mabaya meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini kuwa atatimuliwa mwishoni mwa msimu baada ya kikosi chake kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

City walishindwa kutinga robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuchapwa na Barcelona kwa jumla ya mabao 3-1 huku pia wakiwa nyuma kwa alama sita mbele ya vinara Chelsea katika msimamo wa Ligi Kuu.

Savage amesema anadhani muda wa Pellegrini kuinoa City umefikia ukingoni na kuwapigia chapuo meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti na Diego Simeone wa Atletico Madrid kama makocha wanafaa kuinoa timu hiyo.

Hata hivyo, golikipa wa City Joe Hart amemkingia kifua Pellegrini na kudai kuwa wanamuunga mkono kwa asilimia mia moja kwani aliwasaidia kushinda mataji mawili msimu uliopita.

Pellegrini alishinda taji la Ligi Kuu na Kombe la Ligi msimu uliopita ikiwa ni msimu wake wa kwanza kuinoa City.