Serena Williams afuzu nusu fainali

Haki miliki ya picha AP
Image caption Serena na uso wa amini usiamini

Nyota wa tenesi Serena Williams ametinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya BNP Paribas kwa kumshinda Timea Bacsinszky.

Serena alipata upinzani mkali katika mchezo huo toka kwa mpinzani wake na kuibuka na ushindi wa seti 7-5 6-3.

"nina furaha nimeweza kuendelea kuwepo kwenye mashindano, kitu pekee nachojua nitacheza vizuri zaidi alieleza Serena baada ya ushindi huo.

Katika mchezo mwingine Simona Halep alishinda mchezo wake dhidi ya Carla Suarez Navarro kwa seti 5-7 6-1 6-1, kwa ushindi huo Simona atachuana na Serena Williams katika hatua inayofuata.