Klabu za England hoi kimataifa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Moja ya mechi kati ya Everton na Dynamo

Jana usiku viwanja kadhaa viliwaka moto, katika michuano ya ligi ya Europa wakati timu kadhaa ziliposhuka dimbani katika hatua ya 16 bora. Everton ya England imetupwa nje ya mashindano hayo baada ya kuchapwa bao 5-2 dhidi ya Dynamo Kyiv ya Ukraine, na kufanya matokeo ya jumla kuwa ni 6-4 baada ya mchezo wao wa awali Everton kushinda nyumbani bao 2-1.

AS Roma imeangukia pua baada ya kuchabangwa mabao 3-0 nyumbani pale walipocheza na Fiorentina zote kutoka nchini Italy.Kwa matokoe hayo Roma imetupwa nje kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wao awali.

Nayo Inter Milan ikakwaa kisiki baada kufungwa goli 1-2 dhidi ya Wolfsburg ya Ujeruman na kuondoshwa pia katika mashindano hayo kwa magoli 5-2 baada ya awali kufungwa mabao 3-1, huku Villarreal ikikaangwa goli 1-2 dhidi ya Sevilla na kubwagwa nje kwa goli 5-2 ambapo awali walifungwa goli 3-1.

Mashindano hayo Europa kwa sasa yanaingia katika hatua ya robo fainali.