Brazil kuivaa Ufaransa hapo kesho

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Timu ya Brazil

Timu ya Taifa ya Brazil itapepetana na Ufaransa katika mchezo wa kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya Fifa.

Mchezo huu wa miamba hawa wa soka utachezwa kwenye dimba la Stade de France, Jijini Paris.Ni mchezo muhimu kwa timu zote, Ufaransa wanajianda na michuano ya ulaya itakayofanyika nchini humo mwaka 2016.Huku Brazil wakijiwinda na michuano ya Copa America. Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa mwaka 2013 ambapo Brazil waliichabanga Ufaransa kwa mabao 3-0. mchezo huu utawakutanisha Didier Deschamps na Dunga makocha waliokuwa manahodha wa timu zao wakati wa michuano ya kombe la dunia mwaka 1998 Michezo mingine ya kirafika itakayopigwa hapo kesho ni pamoja na Bahrain na Colombia,huku Chile wakipepetana na Iran.