Lewis Hamilton kuongeza mkataba mpya?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Lewis Hamilton

Timu ya magari yaendayo kasi ya Mercedes ina matumaini ya kumuongezea mkataba dereva wake Lewis Hamilton Hamilton anatarajiwa kusaini mkataba mpya na timu yake unakatiriwa kuwa na thamani ya £40 kwa mwaka kabla ya jumapili ambapo michuano ya Malaysian Grand Prix itaanza timua vumbi. Nyota huyu wa mbio za magari alihudhuria chakula cha mchana katika kambi ya vijana ya Malacca huko Malyasia. Dereva huyu raia wa Uingereza anashikilia nafasi ya kwanza kwa ubora wa madereva wa magari yaendayo kasi ya Fomula1.