Tanzania wapewa mafunzo ya Rugby

Image caption Wanafunzi wa mchezo wa Rugby

Rugby ni miongoni mwa michezo isiyo maarufu nchini Tanzania. Jitihada za kuendeleza mchezo huo zimekuwa zikifanyika na ujio wa vijana wa kimarekani waliotoa mafunzo maalum ya mchezo wa rugby kwa wanafunzi wa shule ya msingi jiji Dar es Salaam kupitia mpango maalum wa 'Bhubesi Pride' ni sehemu ya maendeleo ya mchezo huo.

Wamarekani hao wametokea Kenya na wanaelekea nchini Msumbiji kwa ajili ya programu kama hiyo, yenye lengo la kuendeleza mchezo wa raga kwa nchi za Afrika.mafunzo hayo yametolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi katika nchi 25 za Afrika .

Akizungumzia mafunzo hayo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mapambano, mratibu na mwenyeji wa wamarekani hao kutoka katika kampuni ya GS4, Charles Rwativenga, alisema kuwa hii ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka mitatu kwa wamarekani kuja nchini na kutoa mafunzo hayo.

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo mchezo wa rugby, ama raga haujawa maarufu sana huku timu za Arusha Rhinos, Dar Leopards zikiwa ndio timu kongwe zinazoshiriki lifi kuu huku timu ya taifa ikishiriki mara chache michuano mikubwa ya Afrika.