Walcot asema hajakosana na Wenger

Haki miliki ya picha PA
Image caption Theo walcot

Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot anasema kuwa hajakosana na meneja Arsene Wenger na kuongezea kwamba bado hajaanza mazungumzo ya mkataba mpya na kilabu hiyo.

Mkataba wa Walcot unakamilika mwaka 2016 na Wenger amesema kuwa anatarajia kuwa na mda mrefu wa makubaliano.

''Ripoti zinazosema nimekosana na kocha juu ya kandarasi ni upuzi mtupu'',alisema mchezaji huyo wa miaka 26.

Hatujaanza mazungumzo yoyote juu ya kandarasi yangu na lengo langu kuu ni kufanya vyema katika kilabu hii.