Riadha Tanzania warejea mbio za Nyika

Image caption wanariadha wakiwa mbioni

Timu ya taifa ya riadha ya Tanzania imerejea nyumbani Tanzania baada ya kumalizika kwa michuano ya mbio za Nyika za Dunia iliyofanyika nchini China.

Kocha wa timu hiyo, Fancis John amewasifu wachezaji wake kwa kufanya vizuri miongoni mwa 51 zilizoshiriki.Kenya, kama kawaida yake, ilitawala mbio hizo.

Kenya ni miongoni mwa nchi zinazoongoza katika riadha Afrika na duniani kwa ujumla na wakimbiaji wake, Agnes Tirop (19) na Geoffrey Kamworor wakishinda kwa upande wa wanawake na wanaume.

Kamworor alimaliza mbio za kilomita 12 katika dakika 34 na sekunde 52 mbele ya Mkenya mwenzie, Bedan Karoki, hukun Muktar Edris wa Ethiopia akimaliza wa tatu katika dakika 35 minutes na sekunde 6.

Ismail Juma wa Tanzania alimaliza nafasi ya 9 akitumia muda wa 35:55.