Tiger Woods ashuka kiwango

Haki miliki ya picha Press Association
Image caption Tiger Woods

Waswahili husema hakuna mwanzo usio na mwisho. Hili limedhihirika kwa aliyekuwa kinara kwenye mchezo wa gofu Tiger Woods baada ya kuporomoka katika viwango vya dunia vya mchezo huo na kutolewa nje ya mia bora.

Tukio hili ni la kwanza kumkuta mchezaji huyo katika kipindi chake cha uchezaji. Woods ambaye ni bingwa mara 14 aliingia mia bora kwa mara ya kwanza mwaka 1996 ameweka rekodi ya kuwa bingwa wa dunia kwa wiki 683, lakini sasa ameteremka mpaka nafasi ya 104. Mwenyewe Tiger amesema anamatumaini ya kurejea katika kiwango chake katika shindano kubwa la mwaka la Masters litakaloanza April 9 mwaka huu.