Italy na England watunishiana misuli

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Moja ya mpambano kati ya England na Italy

Pamoja na kuwa miongoni mwa mataifa yenye nguvu kwenye vita ya pili ya dunia,usiku wa kuamkia leo, Italy imekuwa mwenyeji dhidi ya England katika moja ya michezo ya kimataifa ya kirafiki kwa mjibu kalenda ya FIFA.

Kwenye pambano hilo wababe hao walishia kutunishiana misuli tu baada ya kutoka sare ya 1-1. Nayo Uholanzi ililipa kisasi cha fainali za mwaka 2010, baada ya kuisambaratisha Hispania bao 2-0. Ureno wakicheza bila Christian Ronaldo, walikiona cha moto baada ya kuadhibiwa nyumbani bao 2 kwa nunge dhidi ya Cape Verde, huku Sweden wakiichabanga Irani mabao 3-1. Leo hii viwanja viwili vitakuwa tabuni, pale Argentina itakapowavaa Ecuado huku Mexico ikiivaa Paraguay.