Kenya,Namibia zafuzu,Tanzania chini

Image caption Timu ya Kriketi ya Tanzania

Michuano ya Afrika ya kriketi ya Daraja la 1 ( T20) imemalizika nchini Afrika ya Kusini huku Namibia na Kenya zikifuzu kucheza michuano ya T20 ya Dunia ya kufuzu (ICC T20 World Cup Qualifiers ) itakayofanyika katika nchi za Ireland na Scotland baadae mwaka huu.

Licha ya kufungwa na Namibia, ambao ndio mabingwa, Kenya pia imefuzu katika michuano ya kufuzu ya Dunia huku Tanzania ikishuka daraja kutokana na kupoteza mechi zote, ikifungwa na Namibia, Kenya, Uganda na Botswana.

Ukiitoa Tanzania, nchi zote zilizoshiriki zitabaki katika ngazi ya Daraja la 1 kwa Afrika.

Michuano hiyo ya kufuzu ya dunia itahusisha timu kutoka katika mabara mengine ili kugombania nafasi ya kucheza kombe la dunia.

Uganda, ambayo imefanikiwa kubaki katika ligi daraja la 1, ilifungwa na Ghana kwa runs 5 katika michuano iliyofanyika katika uwanja wa Sahara Willowmoore Park.