Arsenal kuchuana na Liverpool

Haki miliki ya picha AP
Image caption Arsenal

Arsenal itamkagua mshambuliaji Danny Welbeck ambaye ana jeraha la goti.

Mikel Arteta ,Alex Oxlaide Chamberlain,Mathieu Debuchy na Abou Diaby hawatachezeshwa licha ya kurudi katika mazoezi,lakini Jack Wilshere huenda akachezeshwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Liverpool

Wachezaji wa Liverpool, nahodha Steven Gerrard na Martin Skrtel wanaanza kuhudumia marufuku yao ya mechi tatu lakini Lucas amerudi baada ya jeraha la paja.

Daniel Sturridge huenda akachezeshwa baada ya kupona jeraha la kiuno naye Raheem Sterling amepona jeraha la kidole cha mguuni lakini Adam Lallana hajulikani iwapo atachezeshwa kutokana na Jeraha la kinena.