Liverpool yamng'ang'ania Raheem Sterling

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Brendan Rodgers

Kocha wa Liverpool ya England Brendan Rodgers, amesema Raheem Sterling hataondoka katika klabu hiyo, msimu wa kiangazi japo kuwa mazungumzo kuhusu mpango mpya kati ya mchezaji huyo na vijogoo hao wa Anfield yamevunjika.

Sterling mwenye umri wa miaka 20 aliiambia BBC kuwa yeye anavutiwa zaidi kutwaa mataji na wala siyo pesa,maneno ya mchezaji huyo yanakuja baada ya kukataa ushawishi wa mkataba wa kitita cha paundi laki 100,000 kwa wiki. “Liverpool ni moja ya vilabu vyenye nguvu katika soka na kama wamiliki hawataki kuuza mchezaji, hawawezi kufanya hivyo” alisema Rodgers.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Raheem Sterling

Raheem amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa awali ambao unamlipa kiasi cha paundi 35,000 kwa wiki.

“ Ni kweli mkazo unapaswa kuwa kwenye soka. Kama matarajio yake ni kushinda mataji ni jambo ambalo linafungamana na kile tunachokifanya sisi” aliongeza Rodgers.

Kocha huyo pia alisema kuwa Liverpool haikumruhusu Sterling kuzungumza na BBC jambo analofikiri ni makosa kufanya mahojiano. ‘‘ atajifunza sisi sote tunafanya makosa katika maisha, haswa tunapokuwa wadogo” alimalizia Brendan.