Tenis kuzikutanisha Nchi za Afrika Misri

Image caption Kijana akijifua katika viwanja vya gymkhana

Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi ni miongoni mwa nchi zitakashiriki michuano ya Afrika ya tenisi kwa vijana chini ya miaka 18 inayoanza wikiendi hii nchini Misri.

Shirikisho la tenisi nchini Tanzania (TTA) limetaja wachezaji watatu watakaoiwakilisha nchi. Wachezaji hao ni Emmanuel Mallya, Frank Mernad na Omary Sulle.

Kocha wa Tanzania, Majuto Majaliwa amesema wamejipanga kufanya vizuri licha ya upinzani kuwa mkubwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kenya, nchi hiyo imechagua pia wachezaji wane ambao ni Stephanie Mbaya, Oliver Kigotho, Kevin Cheruiyot na Sheel Kotecha.

Mbali ya nchi hizo za Afrika ya Mashariki, nchi nyingine za Afrika zinazotegemewa kushiriki ni Tunisia, Morocco, Afrika ya Kusini, Zimbabwe na wenyeji, Misri.