Arsenal yaibana Liverpool,Man U yashinda

Haki miliki ya picha EPA
Image caption manchester United

Arsenal imeimarisha uongozi wao wa kushiriki katika mechi za vilabu bingwa barani Ulaya baada ya kuicharaza Liverpool mabao 4-1 katika uwanja wa Emirates.

The Gunners iliweka wazi lengo lao la kuchukua pointi zote tatu baada ya kufunga mabao matatu ya haraka katika dakika nane za mwisho za kipindi cha kwanza kupitia Hector Bellerin,Mesut Ozil,na Alexi Sanchez huku mshambuliaji Olivier Giroud akipiga msumari wa mwisho wa jeneza la Liverpool alipofunga bao la nne katika kipindi cha pili.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Arsenal

Wakati huohuo Manchester United imeishinda Aston Villa mabao 3-1 na kupanda hadi nafasi ya tatu katika jedwali la ligi ya Uingereza.

Kipa wa Aston Villa Brad Guzan alipangua mkwaju uliopigwa na mlinzi Marcos Rojo lakini alifungwa na Anders Herrera baada ya kazi nzuri kutoka kwa Daley Blind.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption wachezaji wa Liverpool

Wayne Rooney aliongeza bao la pili alipofunga katika kona ya mlingoti wa goli.

Hatahivyo Villa walipata bao la kufutia machozi kupitia mshambuliaji wao Benteke huku Anders Herrera akifunga udhia.