Brendan Rodgers akitetea kikosi chake

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Breandan Rodgers akitetea kikosi chake baada ya kushindwa na Arsenal

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers ameutetea mwelekeo wa kikosi chake baada ya kushindwa mabao 4-1 na timu ya Arsenal.

Mechi hiyo ambayo ni ya pili kwa Liverpool kupoteza mfululizo,inaiwacha timu hiyo ikiwa alama saba nyuma kuweza kufuzu katika michuano ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Hatahivyo Rodgers amesema kuwa mwelekeo wa wachezaji wa timu hiyo ni mzuri

''Tumefanya mikutano mingi kuangazia makosa yetu na lengo la letu la kumaliza katika nne bora'',alisema Rodgers.

Mkufunzi huyo amesema hayo licha ya kusema siku ya jumamosi kwamba hawana hakika iwapo watafuzu kwa kombe la vilabu bingwa Ulaya.