Liverpool kucheza nusu fainali ya FA

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wachezaji wa Liverpool

Wingu lililokuwa limetanda juu ya kilabu ya Liverpool pamoja na meneja wake Brendan Rodgers baada ya kushindwa mara mbili mfulululizo katika mechi za ligi kuu huko Manchester United na Arsenal limeondolewa baada ya timu hiyo kuishinda Blackburn Rovers 1-0 na hivyo kuelekea katika uwanja wa Wembley.

Huku matumaini ya Liverpool kumaliza katika timu nne bora katika ligi ya Uingereza yakididimia, umuhimu wa taji la FA unaimarika na kwamba ushindi huo dhidi ya Blackburn unawakutanisha na Aston Villa katika mechi ya nusu Finali.

Rodgers pia anatarajiwa kuipatia Liverpool taji lao la kwanza tangu ishinde kombe hilo dhidi ya Cardiff chini ya ukufunzi wa Kenny Dalgish mwaka 2012.