Lewis Hamilton atetea taji lake vyema

Haki miliki ya picha AP
Image caption Hamilton akielekea kwenye utepe

Dereva nambari moja duniani Lewis Hamilton wa timu ya Mercedes ameibuka bingwa kwa mara nyingine katika shindano la mbio za magari ya langalanga ya China Grand Prix.

Hamilton aliendesha kwa kasi zaidi na kufanikiwa kupata ubingwa huo huku dereva mwenzake wa timu hiyo Nico Rosberg akimaliza katika nafasiya ya pili.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hamilton akiwa na tuzo la mshindi

Hata hivyo Rosberg amemlalamikia Hamilton kwa kujaribu kumrudisha nyuma katika kumkimbiza Sebastain Vettel wa timu ya Ferrari, madai ambayo yanapingwa vikali na Hamilton.

Nafasi ya tatu ilimwendeaa Sebastain Vettel wa Ferrari huku ya nne ikimangukia Kimi Raikkonen vilevile kutoka timu ya Ferrari.