Phil Nevile amtetea Yaya Toure

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Phil Neville akiwa na Ryan Giggs

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England na Manchester Utd, Phil Neville amemtetea Yaya Toure wa Manchester City kwa kusema kuwa mwanandinga huyo si kikwazo kwa klabu hiyo ya jiji la Manchester kutokana na matokeo mabaya walioyapata katika mchezo wao wa Jumapili. Nevill akizungumza katika mjadala ulifanyika katika studio za BBC, amesema kuwa kocha Manuel Pellegrini ndiye aliyekatika wakati mgumu kutokana na kichapo hicho walichokipata kutoka kwa mahasimu wao wa jiji Manchester Utd, huku akiamini kuwa kocha huyo ndiye wa kulaumiwa kutokana na maamuzi yake yasiozaa matunda aliyoyafanya kuelekea katika mchezo huo.

Manchester City ilibamizwa bao 4-2 na Manchester Utd huku vijana hao wa Etihad wakifikisha michezo sita kupoteza kati ya michezo nane.