Lewis Hamilton ajifagilia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Lewis Hailton

Bingwa wa dunia wa mbio za magari ya langalanga wa timu ya Mercedes Lewis Hamilton amesema yeye yupo vizuri zaidi kiakili kuliko mchezaji mwenzake wa timu hiyo Nico Rosberg. Hamilton anaamini kuwa kisaikolojia yupo juu ya Rosberg katika mapambano ya mataji ya msimu huu.

Lewis ameyasema hayo baada ya Nico Rosberg raia wa Ujerumani kumtuhumu mchezaji huyo kutumia mbinu za kumdhoofisha yeye ili ashinde. ‘‘Mara zote huwa nasema kwamba yeye ni bora kiakili lakini nafikiri mimi nipo bora zaidi mwaka huu” alisema Hamilton.

Rosberg alidai kuwa Hamilton ambaye ni raia wa Uingereza alipunguza mwendo makusudi wiki iliyopita katika shindano la China Grand Prix na kusababisha yeye kumgonga kutokea nyuma japo mjerumani huyo amesema jambo hilo limeshapita na kufutika.