Michuano ya mpira wa pete ni Namibia.

Image caption Wachezaji wa mpira wa pete kutoka Tanzania

Michuano ya Afrika ya mpira wa pete (netball) inategemewa kufanyika nchini Namibia na Tanzania imesema inajipanga kwa ajili ya kushiriki.

Kwa mujibu wa viongozi wa chama cha netball nchini Tanzania (Chaneta), timu ya taifa itachaguliwa muda wowote kwa ajili ya kuanza maandalizi. Michuano hiyo itafanyika mwezi June.

Ushiriki wa Tanzania na timu nyingine utasaidia kupanda viwango vya dunia.

Katika viwango vilivyotolewa na shirikisho la dunia (IFNA) mwezi April mwaka huu, Tanzania ipo nafasi ya 15 na nafasi ya nne katika Afrika.

Malawi ni nchi ya kwanza katika viwango vya Afrika, ikifuatiwa na Afrika ya Kusini na Uganda ikiwa nafasi ya tatu.