CAF yataja wapinzani wa Twiga - Afrika

Image caption Twiga stars viwanjani na shepolopolo ya Zambia

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetaja timu zitakazokwaana na timu ya Twiga Stars ya Tanzania katika fainali za soka za wanawake za Michezo ya Afrika itakayofanyika mwezi Septemba nchini Congo Brazzaville.

Twiga Stars imefanikiwa kucheza fainali hizo baada ya kuitoa timu ya Zambia (Shepolopolo).

Kwa mujibu wa CAF, timu zitakazochuana katika michezo hiyo baada ya kufuzu ni wenyeji Congo (Hosts), Cameroon, Ivory Coast (ambayo imefuzu baada ya Guinea Bissau kujitoa), Ghana, Misri, Nigeria, Afrika ya Kusini na Tanzania

Timu hizo zimefuzu baada ya kupata matokeo yafuatayo:

Nigeria 8-0 Mali (1-1- matokeo ya mechi ya kwanza)

Tanzania 2-3 Zambia (4-2)

Senegal 1-2 Egypt (0-0)

Afrika ya Kusini 5-0 Botswana (0-1)

Cameroon 2-1 Ethiopia (2-1)

Zimbabwe 2-2 Ghana (1-2)