Kocha wa Dortmund kubwaga manyanga.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kocha Jurgen Klopp wa Borrusia Dortmund

Kocha wa klabu ya soka ya Ujerumani Borrusia Dortmund Jurgen Klopp amesema atasitisha mkataba wake na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47, ameomba kukatisha mkataba huo ambao ulipaswa kumalizika mwaka 2018. ‘’ Si hivyo bali nimechoka, sijafanya mawasiliano na timu yoyote na sifikirii kuchukua likizo isiyo na malipo” alisema Klopp.

Kocha huyo ameifundisha Dortmund tangu mwaka 2008 huku akifanikiwa kutwaa mataji mawili ya ligi ya nchi hiyo pamoja na kutinga fainali klabu bingwa Ulaya mwaka 2012-13, japokuwa msimu huu wanaonekana kupepesuka katika msimamo wa ligi ambapo mpaka sasa wapo nafasi ya kumi huku utofauti wa point kati yao na vinara wa ligi hiyo Bayern Munich ikiwa ni point 37.