Messi:Jeraha liliniathiri msimu uliopita

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mshambuliaji wa wa Barcelona Lionel Messi

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amekiri kwamba hakujisikia vyema baada ya kukabiliwa na jeraha.

Raia huyo wa Argentina alikosa kupata taji lolote msimu uliopita mbali na kupoteza mechi ya fainali ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Ujreumani.

Lakini mchezo wake umaimarika tena msimu huu na kuweza kufunga mabao 45 katika mechi 44.

Katika mkesha wa mechi ya robo fainali dhidi ya Paris St-Germain,alisema :Ni mwaka mmoja sasa nimejaribu kusahau haraka yale yaliotokea kupitia juhudi,kazi furaha.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anahitaji bao moja ili kufikisha mabao 400 ya Barcelona wakati ambapo wanachuana dhidi ya PSG kwa mara tatu katika mechi hizo msimu huu.