Etoile kutua Tanzania usiku wa manane

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Etoil du Sahel

Wapinzani wa Yanga timu ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia wanatarajiwa kuwasili saa 9 usiku kuamkia Ijumaa kwa usafiri wa Ndege ya kukodi ya kampuni ya Nouvelair bj 4870 wakiwa na msafara wa watu 56.

Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tunisia (FTF), Krifa Jalel ndiye mkuu wa msafara huo akiwa na Rais wa klabu ya Etoile du Sahel (ESS) Charefeddine Ridha, wachezaji 19, benchi la ufundi lenye watu 13, waandishi wa habari 12 na wanachama 10

Timu ya Etoile du Sahel itafikia katika hoteli ya Ledger Plaza zamani Bahari Beach eneo la Kunduchi, na Ijumaa wanatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Waamuzi wa mchezo huo ni Samwel Chirindiza, Arsenio Marenguka, Celio de Jesus Musabe, Jose Maria Bachide wote kutoka nchini

Msumbuji na walitarajiwa kuwasili mchana wa Alhamisi, huku kamisaa wa mchezo huo Salah Ahmed Mohamed kutokea

nchini Sudan akitarajiwa kuwasili leo jioni na wote watafikia katika hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay.