Nyota ya mafanikio kung'aa kwa Kane?

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Harry Kane akishangilia bao

Mchezaji wa Tottenham Harry Kane ameingia katika orodha ya wachezaji wanne ambao wametajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa kulipwa na ile ya mchezaji bora mwenye umri mdogo katika ligi ya England.

Kipa wa Manchester Utd David De Gea, mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard na kiungo mkabaji wa Liverpool Philippe Coutinho pia wanaweza kushinda tuzo zote mbili. Alexis Sanchez wa Arsenal na Diego Costa wa Chelsea wanatimiza orodha ya wachezaji wakubwa.Nae mchezaji wa timu ya wanawake ya Manchester City Lucy Bronze ambaye ni mshindi wa mwaka jana, ametajwa pia kuwania tuzo hizo kwa upande wa wanawake.

Huku Hazard akiingia katika orodha hiyo ya wakubwa kwa mwaka wa tatu mfululizo japokuwa miaka yote miwili iliyopita akiwa amepoteza na kuchukuliwa na Gareth Bale kabla ya kuhamia Madrid na baadaye kuchukuliwa na Luis Suarez.Ushindi wa Bale wa mwaka 2013 ulifanana na ule wa Andy Gray mnamo mwaka 1977 na ule wa Cristiano Ronaldo kwa kushinda tuzo zote mbili yaani ile ya wakubwa na ile ya mwenye umri mdogo.

De Gea amedhamiria kuwa kipa wa kwanza kushinda tuzo hiyo ambayo kwa mara ya mwisho ilichukuliwa na Peter Shilton mwaka 1977.Kwa upande wa wachezaji vijana wamo pia Raheem Sterling wa Liverpool na Thibaut Courtois kipa wa Chelsea.