Liverpool: hatubagui waislamu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Liverpool FC inafikiria kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya shabiki wake sugu ambaye aliwakebehi mashabiki wawili Waiislamu

Liverpool FC inafikiria kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya shabiki wake sugu ambaye aliwakebehi mashabiki wawili Waiislamu kwa kuswali wakati wa muda wa mapumziko katikati ya mechi.

Shabiki huyo sugu,Stephen Dodd, aliweka picha katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter picha iliyoonesha waislamu wawili wakisujudu .

Waislamu hao wawili Asif Bodi na Abubakar Bhula walitumia kipindi hicho cha mapumziko kuswali kando kando ya ngazi za kuingilia uwanjani.

Picha hiyo ilikuwa na maneno haya;

”waislamu kuswali wakati wa mapumziko ya mechi jana ni fedheha”.

Klabu hiyo ya ligi kuu imeripoti taarifa hizo kwenye kituo cha polisi cha Merseyside baada ya kupata shutuma nyingi.

Baadhi ya mashabiki wa Liverpool katika mitando wa kijamii na vyombo vya habari nchini Uingereza waliichapisha picha hiyo wakati wa mechi ya robo fainali ya kombe la FA Liverpool walipokua wakichuana dhidi ya ya Blackburn Rovers,mchezo uliofanyika tarehe 8 Machi .

Klabu ya Liverpool imewakumbusha mashabiki wake kuwa haitavumilia ubaguzi wa aina yoyote na kuhakikisha kwamba kwamba kuna mazingira salama kwa mashabiki wote bila ya kujali rangi , dini, jinsia , umri, ulemavu au mwelekeo wa kijinsia.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Liverpool inafikiria kumuadhibu shabiki wake aliyewakejeli mashabiki Waislmu

Bodi mwenye umri wa miaka 46 aliiambia jarida la ''the Liverpool Echo'

" Kama Muislamu kipindi kidogo mno cha kuswali sawa tu na ilivyo katika dirisha la uhamisho likipita ndio basi limekwenda''

''Siku hiyo muda wetu wa kuswali ungekamilika kabla ya mechi kumalizika kwa hivyo ilitubidi tuwahi mapema wakati wa mapumziko''.

Kwa kawaida mashabiki wengi hawana ila nasi ila huwa ni tukio linalotegemea hali ilivyo uwanjani.

''Akitokea mtu mmoja ambaye hafurahii basi huenda ikazua tafrani''