Arsenal yatinga fainali ya FA

Image caption Wachezaji wa Arsenal wakisherehekea bao walilofunga dhidi ya Reading

Reading ilikuwa ikicheza kufa na kupona ili kushiriki katika mechi ya fanaili ya kombe la FA katika uwanja wa Wemble,ambayo ni kwa mujibu wa mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger.

Reading ilitoka nyuma na kusawazisha na kufanya mechi hiyo kuchezwa katika mda wa ziada.

Vilvile walishindwa kutumia nafasi muhimu kuilaza Arsenal.

Makosa ya kipa Adam Federic yalipaatia Arsenal ushindi huku mechi hiyo ikikamilika 2-1 kupitia mabao yaliofungwa na mchezaji nyota wa Arsenal Alexei Sanchez