Aston Villa yaipania Arsenal fainali FA

Haki miliki ya picha z
Image caption Tim Sherwood kocha wa Aston Villa aipania Arsenal
Image caption Arsene Wenger

Baada ya Aston Villa kushinda bao 2-1 dhidi ya Liverpool katika mechi ya nusu Fainali michuano ya FA Cup,sasa kocha wa Aston Villa Tim Sherwood anasema wanajinoa kuwakabili Arsenal katika mechi ya fainali.

Hata hivyo amesema kuwa wanatakiwa kujiandaa vilivyo kwani Arsenal katika mechi za awali walizocheza nao waliwahi walipewa kipigo cha 3-0 na 5-0 hivyo akasema maandalizi wanayopaswa kuyafanya si ya mzaha.

Sherwood amesema kuwa kuna kazi kubwa ya kufanyika ya maandalizi kuanzia sasa hadi siku ya May,30mwaka huu.

Tutakachotakiwa kukifanya nikujilinda,lakini wakati huo huo kushambulia na kuhakikisha tunawashinda Arsernal.