Kombe la FA:Aston Villa yaibwaga Liverpool

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Aston Villa yatinga fainali ya FA

Aston Villa imetinga fainali ya kombe la FA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000 baada ya Fabian Delph kufunga bao la pili na la ushindi dhidi ya Liverpool katika mechi ya semi fainali.

Ushindi huo umeiwacha Liverpool bila kitu msimu huu .

Liverpool ilichukua uongozi kupitia Phillipe Coutinho ambaye alivamia lango la Aston Villa kabla ya kucheka na wavu licha ya kukabwa na wachezaji wa Villa.

Lakini Villa walisawazisha kupitia Christian Benteke aliyepata pasi kutoka kwa Delph.

Delph baadaye alifunga bao la pili baada ya kuwapita walinzi wa Liverpool na hivyobasi kutinga fainali ya kombe hilo na Arsenal mnamo tarehe 30 ilioicharaza Reading 2-1 siku ya jumamosi.