Chelsea yailaza Manchester United

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mechi kati ya Chelsea na manchester United iliochezwa katika uwanja wa darajani.Chelsea ilishinda kwa bao moja kwa bila

Mkufunzi wa kilabu ya Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa wachezaji muhimu wa Manchester United walizuia katika mechi iliochezwa kulingana na mahitaji yake.

Kocha huyo sasa anasema kuwa timu yake inaelekea kushinda ligi baada ya kuichapa Manchester United 1-0 katika uwanja wa darajani na kusonga pointi kumi mbele ya Arsenal ambao wako nafasi ya pili.

United ilitawala mchezo na ilikuwa na nafasi nyingi ikilinganishwa na viongozi hao wa ligi.

Mourinho:Tuliandaa mechi hiyo ichezeke ilivyokuwa.ni mechi tuliotarajia na ilichezwa kulingana na mpango wetu.

Chelsea watatawazwa kuwa mabingwa iwapo watashinda dhidi ya Chelsea ama Leicester katika mechi mbili zijazo,baada ya kuishinda Manchester United ambayo iko nafasi ya tatu kupitia bao la Eden Hazard.