FA:Liverpool kuchuana na Aston Villa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Liverpool dhidi ya Aston Villa katika semi fainali ya pili ya kombe la FA

Kocha wa Aston Villa Tim Sherwood amesema kuwa haijulikani iwapo Gabriel Agbonlahor atakabiliana na Jeraha la mguu ili kucheza dhidi ya Liverpool.

Ciaran Clark na Carlos Sanchez ambaye anahudumia marufuku hawatacheza lakini Scott Sinclair na Ashley Wood wamepona .

Jordon Ibe wa Liverpool hatacheza huku Daniel Sturridge akiwa hajulikani kutokana na jeraha baya.

Mamadou Sakho hatacheza kutokana na jeraha la mguu lakini Martin Skirtel na Steve Gerrard wanarudi baada ya kuhudumia marufuku.