Wanariadha 30,00 kushiriki mbio za Boston

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shambulio la Bomu Boston

Zaidi ya wanariadha elfu thelathini watashiriki katika mbio za mwaka huu za masafa marefu za Boston Marathon, miaka miwili baada ya mashambulio mawili ya mabomu, kutokea katika eneo la kumalizia mbio hizo.

Watu watatu waliuawa kwenye shambulio hilo na wengine zaidi ya mia mbili sitini kujeruhiwa.

Siku ya Jumanne, jopo maalum litaanza kuamua ikiwa mmoja wa washambuliaji hao, Dzhokhar Tsarnaev, atahukumiwa adhabu ya kifo.

Wiki mbili zilizopita, alipatikana na hatia ya mashtaka kadhaa ya uhaini ikiwemo kutumia silaha za maangamizi kuua watu watatu katika mbio hizo za marathon, kuwaua afisa wa polisi siku chache baada ya shambulio hilo.