Timu 4 zatinga nusu fainali,Ulaya

Haki miliki ya picha AP
Image caption Javier Hernandez akishangilia goli mbele ya mashabiki wa Real Madrid

Timu nne zimetinga hatua ya nusu fainali katika ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyokamilika hapo jana, baada ya Real Madrid ya Hispania na Juventus ya Uitaliano kufanikiwa kuingia nusu fainali.

Image caption Timu ya Juventus

Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu, Madrid walilazimika kusubiri hadi dakika ya 88, walipopata bao lao la pekee lililotiwa kimia Javier Hernandez almaarufu kama Chicharito,na hivyo kuhitimisha safari ya Atletico Madrid.

Katika msimu uliopita, huko Lisbon Ureno, Atletico walitolewa na Real Madrid katika hatua ya fainali.

Nayo Juventus imezima matumaini ya Monaco ya Ufaransa kwa kulinda bao lake lililofungwa katika mechi ya awali na hapo matokeo ikawa sare ya bila kutofungana. Hata hivyo nyota ni njema kwa Spain ambao sasa wanawakilishwa na timu mbili ambazo ni Real Madrid na Barcelona.