Klabu bigwa ulaya ,Europa kupangwa kesho

Droo ya kupanga ratiba ya nusu fainali ya klabu bigwa na ile ya Europa ligi itafanyika kesho mchana katika mji wa Nyon huko Uswisi.

Robo fainali ya klabu bigwa ulaya ilimalizika jana kwa timu nne kutinga nusu fainali ,mabingwa Watetezi Real Madrid na FC Barcelona Juventus ya Italy na na Mabingwa wa Ujeruman Bayern Munich.

Droo hii ni huru ikimaanisha Timu yeyote inaweza kupangwa na yeyote na hivyo upo uwezekano wa hata timu za nchi moja kwa maana ya Barcelona na Real Madrid wakakutana katika nusu fainali.

Usiku huu Europa ligi watakamilisha Mechi zao za Marudiano za Robo fainali na timu nne washindi zitaingizwa kwenye droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali ambayo pia ni huru bila kujali Utaifa.