Viera apigiwa upatu kumrithi Pellegrini

Image caption Patrick Viera

Patrick Viera anaungwa mkono na wachezaji wengi wa kilabu ya Manchester City kumrithi Manuel Pellegrini iwapo kilabu hiyo itamfuta kazi mkufunzi huyo ambaye ameshindwa kuimarisha matokeo ya kilabu yake.

Maisha ya Pellegrini katika kilabu hiyo ya Etihad yanaangaziwa kufuatia msururu m'baya wa matokeo.

Vieira atakuwa miongoni mwa wanaotazamiwa kumrithi Pellegrini iwapo bodi ya kilabu hiyo itaamua kumpiga kalamu kocha huyo.

Wachezaji wengi wanataka raia huyo wa Ufaransa kupewa uongozi wa kilabu hiyo iwapo Pellegrini atang'atuliwa.

Mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Arsenal anaheshimiwa sana na wachezaji wa kilabu hiyo.

Vilevile kazi yake nzuri na kikosi cha vijana chipukizi katika kilabu hiyo imeonekana na wachezaji hao.